GAVANA ACHANI AWATAKA WENYEJI KUTOKUBALI KUGAWANYWA

Gavana wa Kwale Fatuma Achani amewahimiza wakazi wa Kaunti hiyo kutokubali kugawanywa Kwa misingi ya kikabila na dini.
Akizungumza katika Wadi ya Vanga huko lunga lunga alipoongoza ufunguzi wa shule ya chekechea ya Umba, Achani amesema wakati wa siasa ulipita, hivyo ni wakati sasa wa wakaazi kuungana sawia na viongozi wao ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inafanikishwa.
CUE IN …ACHANI UKABILA
Akiitilia mkazo kauli hiyo Naibu Gavana wa kaunti hiyo Josephat Chirema Kombo amesema Serikali ya Kaunti ya Kwale itawahudumia wananchi wote kwa usawa ili kuzifanikisha ahadi za maendeleo walizotoa wakati kampeni.