WENYEJI WA KAUNTI YA KILIFI WATAKIWA KUFANYA VIPIMO VYA AFYA

Msimamizi wa kituo cha matibabu cha Kijanaheri eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi Daktari Shungu Mathole amewahimiza wenyeji kubadilisha mtindo wa maisha kwa kula vyakula ambavyo havitachangia kwa magonjwa kama ya Moyo.
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu Shungu amesema watu wengi wamekuwa na hulka ya kula vyakula vilivyo na mafuta mengi ambavyo vinachangia kwa wengi wao kuugua ugonjwa wa Moyo hali ambayo imekuwa ikihatarisha maisha yao.
Kulingana na Shungu ili kudhibiti baadhi ya magonjwa ambayo yamekuwa yakichangia kuongezeka kwa maafa ni vyema kwa watu kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuafikia hilo.
Wakati huohuo, ametoa wito kwa jamii kutembelea vituo vya afya mara kwa mara ili kufanyiwa vipimo ili kubaini iwapo wanaugua ugonjwa huo au la ili kupata matibabu.