Wakaazi wa Lunga lunga walioathirika na baa la njaa kaunti ya Kwale wamemtaka rais William Ruto kuwafikishia msaada wa chakula katika eneo hilo.
Wakaazi hao kutoka eneo la Mwereni wamedai hali hiyo imewalazimu wanafunzi kusalia nyumbani kwa sababu ya ukosefu wa chakula.
Wakiongozwa na Kalama Nyawa, wakaazi hao wamesema hawajafanikiwa kupata mazao kufuatia ukosefu wa mvua na uvamizi wa ndovu huku wakisema kuwa chakula cha msaada kilichotolewa na serikali kwa awamu ya kwanza hakijawafikia.
Kwa upande wake afisa wa shirika la kijamii la Inform Action Uba Suleiman ameitaka serikali kupitia shirika la huduma kwa wanyamapori nchini (KWS) kuwakabili ndovu hao wanaochangia uharibifu wa mimea yao shambani.
WENYEJI WA LUNGA LUNGA WAENDELEA KUKABILIWA NA BAA LA NJAA

