Mkufunzi wa zamani wa klabu ya Leicester City Claudio Ranieri amestafu rasmi soka baada ya kuhudumu kama mkufunzi katika vilabu kadhaa Ulaya kwa takriban miaka 30.
Mkufunzi huyo anakumbukwa kwa kuisaidia Leicester City kupanda daraja hadi ligi kuu nchini Uingereza na kushinda kombe la EPL katika msimu wake wa kwanza.
Ranieri kama mkufunzi katika soka la ushindani ameshinda mataji mengi ambayo ni pamoja na kombe la ligi kuu uingereza, Uefa Super Cup, Coppa Italia, Super Copper Italia miongoni mwa mengine.
Hayo yanajiri huku klabu ya Leicester City ikiwa imefanya ujio mpya katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kucheza Championship msimu huu.

