ATALANTA YATWA UBINGWA UROPA

Klabu ya Atalanta ya kule Italia ndio mabingwa wa kombe la Europa msimu huu kwa kuichapa klabu ya Bayer Leverkusen kichapo cha mabao 3-0

Ademola Lookman ndiye aliyeingia kambani mara tatu akifunga ‘hatrick’ katika fainali hiyo.

Kipigo hicho kinakatisha msururu wa kukosa kupoteza mechi kwa Bayer Leverkusen ya Xabi Alonso msimu huu baada ya mechi 51.

Atalanta usiku wa kuamkia leo wamejishindia kombe lao la kwanza tangia 1963, kombe lao la pili katika kipindi cha miaka 116 tangia kuasisiwa kwa klabu hiyo.

Atalanta msimu huu wanakumbukwa pia kwa kuipiga klabu ya Liverpool 3-0 katika kampeni ya kupigania kombe hilo msimu huu katika uwanja wa Anfield.