Klabu ya Gor Mahia sasa imeanza mchakato wa kutafuta mkufunzi mpya katika matayarisho ya mechi zijazo lakini pia msimu ujao ambapo watashiriki sana katika mashindano ya kimataifa ya CAF.
Haya yanajiri baada ya mkufunzi wao wa sasa Johnnathan Mckinstry kusajiliwa kama mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya Gambia baada ya kuwanyakulia ubingwa wao wa 21.
Klabu hiyo pia imekanusha tetesi zinazoihusisha Kogalo kumsajili mkufunzi wa zamani wa klabu ya AFC Leopards Patrick Auussems kwa kile wanachodai kuwa wanalenga mkufunzi ambaye hajawahi kufanya kazi katika vilabu vya Kenya.
Johnathan Mckinstry katika taarifa yake kwa wanahabari mchana wa leo anasema anajivunia mafanikio aliyoyapata katika klabu hiyo licha ya changamoto alizopitia alipokuwa anaichukua klabu hiyo kama kuvungiwa kusajili wachezaji na kadhalika.

