KINADADA WASHAURIWA KUJIHUSISHA NA MICHEZO KILIFI

Ukosefu wa fedha za kuendesha shuhuli za michezo katika klabu ndio sababu kuu inayochangia klabu ya kinadada ya Malindi Starlets kusalia katika ligi ya mkoani kwa misimu miwili mfululizo bila kupanda.

Akizungumza na tama la spoti jioni ya leo katika uwanja wao wa mazoezi wa Alaskan mjini Malindi, Neema Charo ambaye ni mkufunzi wa kinadada hao, anasema hela za kusaidia usafiri wa wachezaji zimewafanya kukosa kuheshimu ratiba za mechi za ugenini jambo ambalo linawashusha alama, hivyo kukosa kupanda daraja kwa miaka miwili mfululizo.

Aidha mkufunzi huyo ametoa wito kwa kinadada wenye kipaji cha soka kujitokeza mashinani na kujisajili na klabu hiyo ili kukuza vipaji vyao, jambo ambalo anataja kuwa litasaidia kuokoa kinadada wengi kwa mimba za mapema lakini pia hatua hiyo kuwasaidia kujiajiri kupitia  michezo.