JOHN MTUTTA MRUTTU APINGA MADAI KUWA ALIFELI WAKATI WA UONGOZI WAKE KAMA GAVANA WA TAITA TAVETA

Aliyekuwa gavana wa kwanza katika kaunti ya Taita Taveta John Mtutta Mruttu amepinga madai kuwa serikali ya kaunti ya Taita Taveta wakati wa uongozi wake ilifeli katika zoezi la ukusanyaji wa ushuru katika masoko yaliyomo mpakani mwa kaunti hiyo ya Taita Taveta na kaunti nyinginezo.

Mruttu amesema utata wa mipaka baina ya kaunti ya Taita Taveta na kaunti zengine unafaa kutatuliwa na kamati maalum inayofaa kubuniwa na bunge la seneti huku akisisitiza kuwa  alihakikisha ukusanyaji wa ushuru kaunti ya Taita Taveta chini ya utawala wake ulizingatia sheria kwa mujibu wa katiba ya humu nchini

Aidha ametoa ushauri kwa serikali ya kaunti iliyo mamlakani kwa sasa kusaka usaidizi kutoka kwa bunge la seneti katika juhudi za kutatua mzozo uliopo kwa sasa kuhusu ukusanyaji wa ushuru baina ya kaunti ya taita taveta na kaunti zengine jirani ikiwemo ile ya Kwale na Makueni.