‘KEN MUST GO!’ ZISHAANZA BANDARI FC

Mkufunzi wa Klabu ya Bandari inayoshiriki Ligi Kuu Hapa Nchini Ken Odhiambo,  anakumbwa Na Shinikizo la Kupigwa Kalamu Kufuatia matokeo Duni na Upande Huo wa Mombasa, akipewa mechi moja ya wikendi Hii dhidi ya Kariobangi Sharks Kutetea Kazi Yake.

Bandari Ilianza Msimu Huu Vizuri ikijiweka Katika nafasi Nzuri ya Kushinda taji La Ligi Kuu, wakitumia kiasi Kikubwa Cha Fedha kwenye Dirisha la Uhamisho Ili Kuboresha Kikosi Chao,

lakini hatua Hizo Ziligonga mwamba kwani kwenye Mkondo wa pili wanamaji hao waliandikisha matokeo Duni, na Hata Kubanduliwa Nje ya Michuano ya FKF Cup.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Bandari Tom Kibwana amethibitisha kuwa uongozi ulimpa Odhiambo mechi mbili kubadilisha Mambo,  Baada ya kupoteza bao moja sufuri dhidi ya Homeboyz siku ya Jumapili  Nyumbani, kocha huyo mwenye leseni ya CAF A anatumai kuwaongoza wachezaji wake kupata ushindi dhidi ya Sharks ili kuokoa kazi yake.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *