Kiongozi wa chama cha PLP (Peoples Liberation Party), Martha Karua amewataka wakenya kujaribu uongozi wa wanawake katika nafasi ya urais mwaka 2027.
Kulingana na Karua kwa mda mrefu, wakenya wamekuwa wakiunga mkono wanaume ambao wamekosa kuwatekelezea maendeleo kama inavyostahili.
Akizungumza kula kaunti ya Isiolo, Karua ametangaza kuwa atawania urais mwaka 2027 na hivyo kutoa wito kwa wakenya kushirikiana katika kumpigia kura kwenye kinyang’anyiro hicho.
Karua amelalamikia suala la kutokuwepo kwa usawa katika zoezi la ugavi wa rasilimali za kitaifa humu nchini.