Wanasiasa Kaunti ya Kwale wameomba jamii katika eneo hilo, kuweka Kando tofauti zao na kushirikiana na viongozi walio mamlakani.
Wakiongozwa na mwakilikishi wadi wa Kasemeni Victor Safari Nyanja, amesema kwamba maeneo mengi ya Kaunti hiyo yamekosa maendeleo kutoka kwa serikali kuu, kutokana na hatua ya baadhi ya viongozi kupinga uongozi walioko mamlakani kitaifa.
Akihutubia jamii katika kaunti hiyo ya Kwale Victor amewarai wananchi hao, kutokubali siasa za mgawanyiko.
Hata hivyo ameiomba jamii kushirikiana na taasisi za elimu ili kupata misaada ya basari.