KAMPUNI YA MAJI, MAWASCO YATAKIWA KUKABILIANA NA VISA VYA WIZI WA MAJI.

Kamati inayoangazia uwekezaji kwenye serikali za kaunti nchini katika bunge la seneti, imeelezea kuridhishwa na mikakati iliyowekwa na kampuni ya kusambaza maji eneo la Malindi, Mawasco, ili kuongeza mapato yake.

Kulingana na mwenyekiti wa kamati hiyo, ambaye pia ni seneta wa kaunti ya Vihigha, Godfrey Osotsi, kampuni ya mawasco imeorodheshwa kuwa kati ya kampuni za maji kitaifa, ambazo zinaongoza kwa kukosa mapato yanayo tokana malipo ya maji, licha ya idadi kubwa ya wananchi wa eneo hili, kunufaika na bidhaa hiyo muhimu.

Akizungumza na wanahabari hapa mjini Malindi, Osotsi amesisitiza haja ya kampuni hiyo, kutekeleza mikakati iliyoweka ili kuhakikisha kuwa inapata faida, kutokana na shughuli za usambazaji wa maji eneo hili la Malindi.

Aidha, ametaja suala la kuwekwa kwa mita za kidijitali kama mojawapo ya mikakati ya kutatua changamoto ya wizi wa maji eneo hili.

Kwa upande wake gavana kaunti ya Kilifi Gideon Maitha Mung’aro, ametoa wito kwa bunge la seneti kuboresha sheria ya maji, ili kusaidia katika kuziba mianya iliyoko, kwenye sheria hiyo ambayo imechangia wale wanaohusika na wizi wa maji kukosa kupewa adhabu kali wanapofikishwa mahakamani.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *