Gavana wa Kaunti ya Lamu Isaa Abdallah Timammy amewataka maafisa wa polisi waliohudumu kwa muda mrefu Kaunti hiyo kuhamishwa.
Timammy akidokeza kuwa maafisa hao, hupitia wakati mgumu, kwani wakati mwingi wamekuwa wakikabiliana na magaidi wa Alshabaab.
Gavana huyo ameongeza kuwa maafisa hao wanafaa kupandishwa vyeo ili kunufaika na jitihada zao za kuhakikishia wananchi wa kaunti hiyo usalama wao.
Kauli ya Timammy imeungwa na Mbunge wa Lamu mashariki Ruweida obo ambaye ameitaka idara ya usalama kuwaangazia maafisa hao wa polisi wanaoshika doria kaunti hiyo.