Wito umetolewa kwa bunge la seneti kusaidia serikali ya kaunti ya Kilifi kupokea malipo yake ya zaidi ya shilingi milioni mia tatu, kutoka kwa bima ya afya ya zamani NHIF na ile ya sasa ya SHIF.
Kulingana na gavana wa kaunti ya Kilifi, Gideon Maitha Mung’aro, licha ya wakaazi wa kaunti ya Kilifi kuendelea kupokea huduma za afya kwa kutumia SHA, mamlaka hiyo ya bima mpya ya afya, imekosa kulipa serikali ya kaunti hii fedha zake.
Akizungumza wakati wa zaira ya kamati ya bunge la seneti, inayo angazia uwekezaji kwenye serikali za kaunti nchini, Mung’aro amesema deni hilo limechangia pakubwa kutatizika kwa shughuli za utoaji wa huduma za afya kaunti hii.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo, ambaye pia ni seneta wa kaunti ya Vihigha, Godfrey Osotsi, ameahidi kufuatilia suala hilo, ili kuhakikisha kuwa serikali ya kaunti ya Kilifi, inapata fedha zake kutoka kwa NHIF na SHIF.