Serikali ya kaunti ya Lamu imetakiwa kuimarisha na kuboresha viwanja vya michezo ukiwemo uwanja ulioko kisiwani Amu ili vijana waweze kukuza talanta zao.
Wito huo umetolewa na viongozi mbalimbali wakiwemo wadau wa masuala ya soka katika uwanja huo wa michezo wa sports kisiwani Amu.
Kwa sasa zaidi ya timu 17 ikiwemo klabu ya Yanga, ziwani youth, kishada, sparky youth zinatarajiwa kucheza mechi zake katika uwanja huo wa sports kisiwani Amu baada ya timu ya Deep Sea ambayo ni timu ya kaunti ya Lamu kupanda daraja kutoka ligi ya mkoa hadi daraja la pili kitaifa.
Hassan Athman ni mkufunzi mkuu wa klabu ya Omax na anaeleza kutamaushwa kwake na uwanja huo wa Sports.
Mwenyekiti wa shirikisho la soka katika kaunti ya Lamu Fuad Ali ameeleza kuridhika na hatua ya vilabu kujisajili na shirikisho la fkf tawi la Lamu na jambo hilo limechangia vilabu vya kaunti mbali mbali kuzuru Lamu baada ya kipindi kirefu kwa sasa.

