Afisa wa nyanjani wa shirika la kijamii la KIUNGA YOUTH BUNGE kaunti ya Lamu Moses Maina amethibitisha kuwa wameanzisha kampeni dhidi ya ukeketaji katika sehemu za mashinani kaunti ya Lamu.
Maina amesema wamechukua hatua hiyo kutokana na kile ambacho anadai kuchangiwa na ongezeko la visa vya ukeketaji na dhuluma za kijinsia katika kaunti hiyo.
Aidha, amesema watawashirikisha wadau mbalimbali kama wanawake walioko mashinani ili kudhibiti visa hivyo katika kaunti ya Lamu.
Kwa upande wake afisa wa kifungo cha nje katika mahakama ya Mpeketoni kaunti ya Lamu Khadija Mohammed amewataka wakaazi kuripoti visa vya dhuluma za kijinsia ili wahusika wakabiliwe kwa mujibu wa sheria.
VISA VYA UKEKETAJI VINGALI VINAENDELEZWA KWENYE KAUNTI YA LAMU

