Timu ya taifa ya Junior starlets ambayo iko Uhispania katika kambi ya kujitayarisha kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Dunia ya kinadada jana ilisajili ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya klabu ya kinadada ya Intercity Femenino.
Ni mechi ambayo inawafanya Junior starlets wanaoongozwa na kocha Mildred Cheche inazidi kujiandaa kwa World Cup igakayoanza tarehe 16 October huko Dominica Republic
Valerine Nekesa alitangulia kufunga dakika ya 18, akitumia vyema pasi ya Joan Ogola pembeni. Hata hivyo, CF Intercity Femenino walipata bao la kusawazisha kabla ya muda wa mapumziko, wakisawazisha bao hilo kuwa 1-1 katika dakika ya 45.
Kipindi cha pili, Quinter Odiwuor alirejesha uongozi wa Starlets kwa shuti kali la pekee lililopita wavuni, na kufanya matokeo kuwa 2-1. Mchezo ulipokuwa ukiendelea, Lorna Faith aliongeza bao la kuongoza hadi 3-1 katika dakika ya 86 kwa shuti kali la juu la kona. Hatimaye, Valencia Joy Angela aliongeza mguso wa mwisho, akipachika bao la nne baada ya jaribio la awali la Jane Kweyu, kuhitimisha bao 4-1.
Leo Junior starlets wanasafiri kuelekea Domicican republic ambako watashiriki mechi yao ya mwisho ya kirafiki kabla ya mashindano kuanza rasmi

