Timu ya taifa ya Junior starlets ambayo iko Uhispania kwa matayarisho ya mwisho kuelekea Kombe la Dunia katika taifa ya Dominica Republic usiku wa kuamkia leo imeshiriki mechi ya kirafiki ili kuzidi kujinoa.
Imekipiga dhidi ya Valencia Women na kushinda kwa bao 4-1.
Mshambuliaji Valerie Nekesa ametia wavuni mabao mawili sawa na lindey Atieno ambaye pia amefunga mabao mawili.
Junior starlets inayoongozwa na kocha Mildred Cheche itashiriki katika mashindano ya fifa ya Kombe la Dunia mashindano yatakayoanza tarehe 16 mwezi octoba mpaka November 3
Izidi kukumbukwa hii ndio timu ya kwanza katika historia ya soka la Kenya kuwai kushiriki mashindano ya Kombe la dunia

