TOM LANGO AAPA KUPIGANIA TIMU ZA KILIFI

Mwaniaji wa uenyekiti wa Fkf katika kaunti ya Kilifi Tom Lango amethibitisha kuwa analenga kutetea vilabu vya kaunti hiyo dhidi ya kile anachokitaja kuwa maonevu kutoka ofisi ya Mombasa.

Kulingana na Lango ni kuwa Mwenyekiti wa sasa Dickson Angore hajakuwa akitetea timu, za Kilifi vilivyo jambo ambalo limesababisha timu kama Maji Bombers na Furunzi Fc zishuke katika kipindi chake.

”Timu kama Furunzi na Maji Bombers kushuka zilinihuzunisha sana, sikufurahia jinsi zilikosa utetezi. Ingekuwa ni mimi hazingeshuka’ alisema Tom

Kwa sasa mgombeaji mkuu anayepingana na Tom Lango ni Mwenyekiti wa sasa Dickson Angore. Kampeni kwa sasa za endelea huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi November