JUNIOR STARLETS YAFUZU RAUNDI YA TATU RAHISI AJAB!

Kikosi cha taifa cha soka kwa wasichana chini ya miaka 17 Junior Starlets ni rasmi kuwa sasa wamefuzu kwenye raundi ya tatu ya mechi za kuwania kufuzu kwa makala ya mwaka huu ya kombe la dunia.
Hii ni baada ya jana shirikisho la soka barani Afrika CAF kuthibitisha rasmi kujiondoa kwa timu ya DR Congo kwa mechi hizo, huku ikiwa ndiyo waliokuwa wamenyane na Kenya kwenye mechi za mikondo miwili raundi ya pili zilizokuwa zisakatwe Februari tarehe nne ambayo ni jana na 11 mtawalia.
Kenya sasa itapambana na mshindi baina ya Afrika Kusini na Ethiopia kwenye raundi ya tatu.
Mechi hizo za nyumbani na ugenini zitachezwa tarehe 10 mwezi Mei na marudiano tarehe 19 mwezi Mei mwaka huu.
Kutokana na hatua hiyo, kambi ya mazoezi ya timu hiyo imevunjwa kuruhusu wachezaji kurejea shuleni na vilabu wanamochezea.