Mkufunzi Kenedy Rimba ameeleza kufurahishwa kwake na klabu yake ya Bosuster kupanda daraja mpaka hili ya kaunti ya kilifi baada ya jana kusajili ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fundisa FC katika fainali ya Mini League ilochezwa huko Magarini.
Mkufunzi Rimba anasema ameridhika kwa klabu yake kupata fursa ya kipekee kurudi tena katika ligi ya kaunti baada ya kushushwa na FKF kutokana na makosa yalotokea kipindi cha nyuma na kuwafanya kuanza safari katika ligi ya eneo bunge la magarini tena.
”Kwa sasa vijana wako tayari na wako na hamu sana ya kucheza ligi ya kaunti msimu ujao. Tulishuka tu kwa sababu ya makosa madogo lakini sasa wapinzani wanafaa wajue kwamba tunakuja na ubaya.” Alisema Rimba.
Kulingana na mkufunzi huyo ni kuwa klabu hiyo kwa sasa inalenga kuwinda talanta za wachezaji ili kukiboresha hata zaidi kikosi chao akithibitisha kuwa Bosuster inahamu sana ya kushiriki katika ya kaunti.

