Elmond Kasaya hatimaye alifunga bao lake la kwanza katika klabu ya 3K baada ya kusajiliwa kutoka SS Assad ya kaunti ya kwale klabu inayoshiriki katika ligi ya kitaifa ya Super League.
Dakika 16 pekee zilimtosha kufanya hivyo baada ya kuletwa kama mchezaji wa akiba kwenye mechi ambayo ilikuwa inawakutanisha na Simba Apparel mechi ambayo iliisha kwa bao 1-0.
Kufikia sasa Kasaya amecheza mechi mbili pekee katika ligi ya daraja la kwanza baada ya kusajiliwa na klabu hiyo ya 3K yenye makazi yake huko Embu, klabu inayoongozwa na mkufunzi Francis Chege
Kwa sasa 3K inalenga kuzidi kuandikisha matokeo bora msimu huu na angalau kupanda daraja msimu ujao baada ya kufanya usajili wa kufana katika dirisha la usajili la mwaka huu.

