HAKIMI ATUNUKIWA UARABUNI

Difenda wa timu ya taifa ya morocco lakini pia klabu ya Paris Saint Germain Achraf Hakimi ametuzwa kama mwanaspoti bora wa mataifa ya kiarabu wa mwaka 2022.

Beki huyo wa kupanda na kushuka mwenye umri wa miaka 24 alituzwa kwenye mji mkuu Riyadh kwenye sherehe za kukumbuka taifa hilo kwenye masuala ya ndani.

Hakimi ameisaidia timu ya taifa ya Morocco kuingia katika hatua ya robo fainali lakini pia kuweka rekodi ulimwenguni kuwa taifa la kwanza afrika kuingia robo fainali ya mashindano ya kombe la dunia.