Bondia wa Kenya Rayton Okwiri amesaini rasmi mkataba wa udhamini na kampuni ya finix Casino.Kampuni hiyo imethibitisha kwamba itamdhamini Okwiri kwa lengo la kumfanikisho mchezaji huyo ndani na nje ya ulingo.
Hii inatokana na kwamba mabondia wengi wamekuwa wakifeli kufikia vilele vya uwezo wao baada ya kukumbwa na changamoto za ndani na nje ya uwanja.
Ikumbukwe kwamba Okwiri alikuwa bondia aliyemlaza Ally Ndaro kutoka Tanzania jumamoja lilopita katika ulingo ulioko KICC jijini Nairobi katika pambano la kwanza kabla ya Mandonga kutoka Tanzania kuchukua ushindi dhidi ya Daniel Wanyonyi katika pambano la pili.

