Nguli wa mchezo wa raga nchini Kenya Collins Injera amestafu rasmi mchezo huo baada ya kurindima raga ya ushindani kwa kipindi cha miaka 17.
Injera amethibitisha hayo na anaachana na mchezo huo akiwa na rekodi ya try 279, try ambazo katika historia ya raga za wachezaji saba kila upande anasimama katika nafasi ya pili.
Mshindi huyo wa tuzo la mchezaji bora wa mwaka 2009 wa Kenya, ameshauri serikali kuwaenzi wachezaji kwa heshima zaidi wanapostafu hasa wachezaji wa riadha ambao wameletea taifa hili sifa kimataifa.

