GRAHAM POTTER AKUBALI KUWA MKUFUNZI MPYA WA CHELSEA

Mkufunzi wa klabu ya Brighton inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza Graham Potter amekubali kuwa mkufunzi mpya wa klabu ya Chelsea baada ya kufutwa kazi kwa mkufunzi wa klabu hiyo Thomas Tuchel kutokana na matokeo mabay tangia kuanza kwa msimu huu.

Wamiliki wa klabu hiyo ya darajani Stamford bridge tayari wanaripotiwa kufanya mazungumzo na mkufunzi huyo wa Brighton na uhamisho huo huenda ukaharakishwa kuona kwamba klabu hiyo inapata mkufunzi kabla ya mechi ya wikendi hii watakapokuwa wanavaana na Fulham.

Hata hivyo kabla ya Todd Boehly ambaye anaongoza klabu hiyo kusaka mkufunzi mpya awali walikuwa wamefanya mazungumzo na mkufunzi wa zamani wa klabu ya real Madrid Zinadine Zidane, mwengine akiwa ni Brendan Rogers wa Leicester city na mkufunzi wa zamani wa Totenham hotspers mwite Mauricio Pochetino.

Tomas Tuchel alifutwa kazi hapo jana baada ya kushindwa mechi tatu msimu huu ikiwemo ya punde zaidi Chelsea ilipotandikwa kichapo cha bao 1-0 na Dinamo Zagreb katika mechi ya kwanza ya makundi ya klabu bingwa ulaya.