Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya FKF ya kinadada nchini Kenya Vihiga Queens sasa watategemea sajili zao mpya msimu ujao katika harakati ya kutetea ubingwa wao.
Vihiga Queens waliomaliza msimu uliopita bila kupioteza mechi hata moja wamesajili wachezaji sita watakaowasaidia akiwemo Ivy Makhoha kutoka Bunyore Starlets, Eunice Musila wa shule ya upili ya kinadada ya Mwira, na Diana Sigei, Fenny Monchari na Edith Ethycate wote wakitokea klabu ya Solasa Stima Quuens.
Kulingana na mkufunzi wa klabu hiyo Boniface Nyamunyamu ni kuwa kwa sasa wanasubiri mchezaji mmoja kutoka Uganda ajiunge nao na atakuwa mchezaji wa pekee wa kimataifa klabuni hapo.

