Sasa ni rasmi kuwa Ammason Jeffa Kingi ndiye spika wa bunge la seneti. Ammason Jeffa Kingi amepata jumla ya kura 46 kutoka kwa maseneta walioshiriki upigaji kura.
Licha ya wajumbe wanaoegemea upande wa azimio la umoja kutaka zoezi hilo liahirishwe mbali na swala kuwa mwaniaji wao wa wadhfa huo Kalonzo Musyoka kujiondoa kwenye kipute hicho.
Huyu hapa Ammason Kingi akichukua kiapo kabla ya kuchukua rasmi nafasi hiyo ya uspika katika bunge la seneti.
Kingi anaweka historia ya kuwa spika wa kwanza wa bunge la seneti kutoka ukanda wa pwani hususan kaunti ya Kilifi.
AMASON KINGI NDIYE SPIKA MPYA KATIKA BUNGE LA SENETI

