GOR MAHIA KUTOCHEZA MASHINDANO YA CAF

Ni rasmi sasa kuwa Gor Mahia haitashiriki katika mashindano ya kimataifa ya CAF Champions League msimu wa mwaka 2023/2024 licha ya kuibuka mabingwa wa ligi ya FKF hapa nchini Kenya.

Mchana wa leo dro ya mashindano hayo imefanywa katika makao makuu ya CAF jijini Cairo katika taifa la Misri na Gor Mahia imekosa nafasi katika droo ambayo imefanyika.

Haya yanajiri baada ya mwenyekiti wa klabu ya Gor Mahia Ambrose Rachier  kuomba CAF kubatilisha uamuzi wake wa kuifungia klabu hiyo baada ya kukamilisha malipo ya wachezaji waliokuwa wanadai hela Gor Mahia siku ya jumapili.

Wakati hayo yakijiri klabu ya Kakamega Homeboyz imeratibiwa kuanza mashindano ya kombe la CAF Confederation dhidi ya El Hilal nchini Libya mwezi ujao.

Kakamega walifuzu kucheza mashindano hayo baada ya kushinda kombe la shirikisho la FKF mwezi Juni walipovaana na Tusker katika fainali na kushinda ubingwa huo kwa ushindi wa bao 1-0.