MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA YAZIDI KURINDIMA KWA KINADADA

Mashindano ya kombe la dunia yameendelea na mechi tatu zimechezwa ambapo mapema leo  Italia wamesajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Argentina.

Mechi nyingine ambayo imetamatika hivi punde ni ile ya Ujerumani dhidi ya Morocco. Ujerumani wamesajili ushindi wa mabao 5-0.

Timu ya taifa ya Brazil imesajili ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya timu ya taifa ya Panama iliyochezwa mwendo wa saa nane. Kwa sasa mashindano haya ya mataifa 32 yanaendelea katika hatua ya makundi na yalianza rasmi tarehe 20 mwezi July.

Mashindano haya ya kombe la dunia kwa upande wa kina dada yanaendelea katika taifa la New Zeeland pamoja na Australia.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *