ZIWANI YOUTH YAPATA PIGO

Klabu ya Ziwani Youth sasa imepata pigo baada ya mchezaji wake mmoja kulazimika kukaa nje kwa takriban mwezi mmoja kutokana na jeraha la goti.

Mohamed Abongo ambaye ni beki wa kushoto wa klabu hiyo ya kaunti ya Mombasa inayoshiriki katika ligi ya daraja la pili kitaifa alipata jeraha hiyo walipokuwa wanavaana na klabu ya Yanga Fc wikendi ilopita mechi ambayo Ziwani walipoteza Ugenini kwa mabao 2-1.

Katika taarifa aliyoichapisha Abongo kwenye mtandano wa Facebook amesema kwamba alifanyiwa matibabu na kwa mujibu wa daktrari huenda akarudi katika hali sawa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.