GOR MAHIA KUINGIA SOKONI

Klabu ya Gor Mahia ambao ni mabingwa watetezi katika ligi ya fkf nchini Kenya wanalenga kuboresha kikosi chao kwa lengo la kutetea ubingwa huo kupitia dirisha la uhamisho ambalo litakuwa wazi kuanzia Jtarehe 31 mwezi huu, dirisha ambalo litafungwa rasmi tarehe 28 mwezi February.

Raymond Oruo ambaye ni afisa mkuu mtendaji wa Kogalo anasema msimu huu wa uhamsiho watashiriki vilivyo ili kuimarisha kila idara za kikosi hicho kuelekea sehemu ya pili ya ligi msimu huu.

Taarifa zasema Kogalo inawalenga beki wa zamani wa Gor, Dennis Ng’ang’a ambaye alihama klabu hiyo miaka miwili iliyopita na kujiunga na wababe wa Zambia Zanaco.

Ng’ang’a amekuwa akifanya mazoezi na timu hiyo kwa muda sasa chini ya uangalizi wa benchi la ufundi, na iwapo ataonyesha kiwango kizuri, atasajiliwa tena.

Hivi majuzi Gor Mahia waliongeza kandarasi za wachezaji wawili waliokaa muda mrefu zaidi, Philemon Otieno na Ernest Wendo hadi mwisho wa msimu – kandarasi zao zilikuwa zimeisha Januari hii.