TUME YA EACC YAAHIDI KUWAKABILI KISHERIA WAFISADI KWENYE IDARA YA MAHAKAMA NCHINI.

Tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi nchini EACC, imesema kuwa imeanzisha uchunguzi dhidi ya ufisadi unaodaiwa kuendelezwa na wafanyakazi wa tume ya idara ya mahakama JSC.

Kwa mujibu wa EACC, hatua hiyo imetokana na suala la wakenya kulalamikia ongezeko la idadi ya wafanyakazi wa idara hiyo, ambao wamekuwa wakihusika kwenye visa vya ufisadi na kuchangia walalamishi wengi kukosa haki.

Akizungumza na wanahabari mwenyekiti wa tume ya EACC, Askofu David Oginde, amesema kuwa watahakikisha wale watakao patikana na hatia ya kushiriki ufisadi katika idara ya mahakamam wanakabiliwa kwa mujibu wa sheria.

Oginde amehojikuwa idara ya mahakama, inapaswa kuwa huru na yenye kuendekeza maadili ya hali ya juu, ambayo pia yanapinga ufisadi kwenye jamii.