Wizara ya afya nchini imenunua dozi milioni 2.34 za chanjo ya BCG, inayo chanjwa watoto ili kuwalinda dhidi ya kupata maradhi ya kifua kikuu.
Akithibitisha hilo mkurugenzi mkuu katika idara ya afya Dkt Patrick Amoth, amesema kuwa jumla ya chanjo elfu 234, zimesalia katika hifadhi ya kitaifa, ili kuhakikisha hakishuhudiwa uhaba wa chanjo hizo humu nchini.
Mkurugenzi huyo amesema tayari wizara ya afya, imeanza shughuli za kusambaza chanjo hizo katika kaunti mbali mbali za taifa hili.
Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari kule Nairobi, Dktr Amoth amesema kuwa miongoni mwa kaunti ambazo zitapokea chanjo hiyo ni Nairobi, Mombasa, Kisumu, Kakamega, Meru, Nyeri, Garissa, Eldoret na zingine nyingi.
Aidha, Amoth ameongeza kuwa bado taifa hili, linatarajiwa kupokea chanjo zaidi za kuzuia maradhi mengine mengi, huku akitoa wito kwa serikali za kaunti nchini, kuhakikisha kuwa zinaendeleza mikakati ya kuwachanja watoto chanjo hizo.

