Huenda hali ya soka katika kaunti ya Lamu ikazidi kuwa mbaya kutokana na kusambaratika kwa utendakazi wa shirikihso la soka la fkf katika gatuzi hilo.
Vilabu vingi vya soka Lamu vimeshindwa kuendelea na mashindano ya shirikihso kutokana na gharama kubwa ya kusimamia mechi zao. Hivi punde zaidi ni klabu ya Deep Sea na King Loyal zilijitoa kwenye mashindano ya ligi za fkf kwa kile kinachotajwa kuwa ukata wa kifedha huku vilabu zaidi vilisadikika kupanga kujiondoa kwenye ligi za fkf.
Fuad Ali refa mkongwe kule Lamu amethibitishia Tama La SPoti kupitia njia ya simu kuwa kwa sasa Lamu hakuna shughuli zozote za FKF zinazoendelea licha ya uchaguzi kufanyika katika gatuzi hilo mwishoni mwa mwaka jana.
Kulingana na Fuad, Lamu wamekuwa wakitumia muungano wa soka maarufu kama Football Association badala ya fkf na muungano huo haujakuwa ukifanya kazi katika kaunti nzima.
Umbali wa kaunti ya Lamu na kaunti nyingine ambako mashindano ya ligi za fkf hufanyika ni kati ya mambo ambayo pia yanachangia timu nyingi kujiondoa kwenye ligi za fkf.

