Mkufunzi wa zamani wa klabu ya Young Bulls Ali Said Gaucho anatarajiwa kuchukua mikoba kama kocha mkuu wa Malindi United kuanzia msimu jana.
Gaucho ambaye alijiunga na klabu hiyo msimu jana sasa ana kibarua cha kuirudisha klabu hiyo katika ligi ya daraja la kwanza kitaifa.
Kwa sasa anaendelea kunoa vijana wa klabu hiyo inayomilikiwa na mwakikishi wadi wa mji wa Malindi Rashid Odhiambo katika uwanja wa Kagombani Katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi Uwanja ambao ndio mechi za nyumbani za klabu hiyo zifafanyika msimu ujao.
Haya yanajiri baada ya mkataba wa kukodi uwanja wa Alaskan kutamatika mwisho wa msimu uliopita na sasa Alaskan Kulingana na taarifa utakuwa uwanja wa nyumbani wa klabu ya Kisumu Ndogo United

