Klabu ya mji wa Malindi Kisumu Ndogo United imefanya zoezi la majaribio ya wachezaji wa lengo la kuwinda talanta ambazo zitaimarisha kikosi hicho zaidi kuelekea msimu mpya wa Ligi ya mkoa.
Kulingana na kocha Jackson Kalinga ambaye ni Kati ya makocha waliokuwa wanasimamia zoezi hilo ni kuwa vijana wengi kutoka sehemu mbali wamejitokeza huku akitarajia wengine zaidi kutoka sehem mbalimbali za taifa hili.
Kalinga amethibitisha kwa Tama La Spoti kuwa klabu hiyo ambayo kwa sasa inasimamiwa na Ali Best inaundwa kwa ubora ili kuleta ushindani wa ligi msimu ujao huku tayari hii leo zoezi la leo na taarifa za wachezaji kutaka kujiunga na timu hiyo kutoka sehemu za mbali likionyesha kuwa ni kikosi kitakachokuwa na nguvu kwenye soka la mkoa huu.

