FURUNZI FC YALALAMIKA MAONEVU YA MAREFA LIGINI

Mkufunzi wa klabu ya Furunzi FC Nero Chishenga amelalamikia maamuzi mabaya ya refa wa mechi ya jana ya vijana wake walipokuwa wanashuka dimbani dhidi ya klabu ya Ashton Rangers katika uwanja wa Prison eneo bunge la Malindi.

Kulingana na Nero ni kwamba refa wa mechi hiyo aliwanyima penalty mbili za wazi maamuzi yalopelekea vijana wake kupoteza mechi yao ya nyumbani kwa mabao 4-3.

Akizungumza na Tama La Spoti mkufunzi huyo amekashifu uongozi wa fkf katika ligi ya daraja la pili kitaifa kwa kile anachotaja kama mapendeleo kwa marefa wa Mombasa katika mechi za kaunti ya Kilifi ikizingatiwa kwamba kaunti hii pia ina marefa wenye uzoefu wa kuchezesha mechi za ngazi za juu kitaifa.

Kwenye matokeo mengine ya ligi ya daraja la pili kitaifa ni kwamba Omax ya Mombasa walizidisha msururu wa matokeo mazuri kwa kuitandika Mariakani fc kichapo cha mabao 3-0 katika uwanja wa ugenini.

Samburu Lions wakiwa ugenini walisajili ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sparky Youth wakati kishada ikiitandika Ziwani Youth kipigo cha mabao 2-1.
Klabu ya mjanaheri eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi waite Beach Bay walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya klabu ya Inter Dabaso.