Klabu ya Malindi Progressive kutoka Malindi, klabu inayocheza ligi ya daraja la kwanza kitaifa yalenga kuanza mchakato wa kutafuta haki baada ya wasimamizi wa mechi yao jana kuisitisha na kupeana alama tatu na mabao mawili kwa wageni Balaji Epz.
Kulingana na taarifa zilizofikia Tama La Spoti ni kwamba mechi hiyo ilisimamishwa na wenyeji Progressive kuadhibiwa kwa kuzawadi wapinzani alama tatu baada ya wenyeji kukosa kuweka mazingira ya kiafya ya kutosha katika mechi hiyo.
Benard Lusi ambaye ni nahodha wa klabu hiyo ameambia Tama la Spoti kwamba magari ya ambulensi yaliyowasilishwa uwanjani yalikosa vifaa vya kutosha jambo ambalo lilichochea wasimmizi kusimamisha mechi hiyo baada ya ukaguzi.

