Katika ligi ya uhispania ni kwamba Barcelona wamerefusha pengo lao na nafasi ya pili Real Madrid hadi alama 8 ikiwaweka wanakatelonya hao katika nafasi nzuri ya kugombania ubingwa msimu huu.
Hii ni baada ya jana kuitandika klabu ya Cadiz kichapo cha mabao 2-0 katika mechi ambayo Sergio Roberto aliingia kimyani dakika ya 43 na hatimaye kuumpa asisti Robert Lewandoski ambaye alifunga bao lake la 15 la laliga msimu huu.
Kwa sasa Barcelona inaongoza ligi wakiwa na alama 59, Real Madrid ikisimama katika nafasi ya pili na alama 51.
Real Sociodad pamoja na Atletico Madrid zinafuata nafasi ya tatu na nne wakiwa na alama 43 na 41 mtawalia.

