Mchezaji wa timu ya Uingereza na klabu ya Manchester City Phil Foden ameshinda tuzo la mchezaji bora wa muungano wa wachezaji wa kulipwa ama ukipenda wale wanaofanya uchezaji soka kama kazi.
Foden mwenye umri wa miaka 24 ameshinda tuzo hiyo baada ya kuisaidia Manchester City kushinda kombe lake la nne mfululizo msimu uliopita katika EPL
Kwenye ligi kuu Uingereza msimu uliopita Foden alifunga mabao 19 na kutoa pasi za nane mabao na kuisaidia City ya mkufunzi Pep Guardiola kushinda ubingwa huo.
Foden tayari ametangaza azma yake ya kupigania ubingwa wa tano mfululizo katika ligi kuu Uingereza.
Katika kushinda tuzo hiyo Foden amemshinda wachezaji wenza wa Man City akiwemo Rodri na Erling Haaland, mchezaji wa Chelsea Cole Palmer, Martin Odergard wa Arsenal miongoni mwa wengine waliokuwa wanapambania tuzo hiyo mwaka huu

