Timu ya kaunti ya Kilifi inayoshiriki katika mashindano ya dola super cup katika kaunti ya Mombasa kwenye mashindano ya kimkoa imefuzu kutinga semi fainali ya mashindano hayo hii leo baada ya kuandikisha matokeo mazuri.
Timu hiyo imefuzu katika hatua ya robo fainali baada ya kuipiga timu ya kwale A kichapo cha mabao 2-0. Mabao yote mawili katika mechi hiyo yamefungwa na Feiswal Dzuya, mchezaji anayetokea Magarini na anachezea klabu ya ligi ya mkoa GFC.
Hizi hapa ni baadhi ya kauli ya mashabiki walioshuhudia Kilifi ikifuzu semi fainali na wameonyesha matumaini makubwa ya kubeba ubingwa.
Kwale B pia nayo imefuzu kuingia semi fainali baada ya kuichakaza Taita Taveta kichapo cha mabao 3-0.
Kilele cha mashindano haya ni Jumapili ambapo mshindi wa soka la pwani la mashindano haya yanayodhaminiwa na kampuni ya Dola atatuzwa Milioni moja pesa taslimu.

