Vilabu vinne vinavyoshiriki ligi ya soka ya FKF kaunti ya Tana River vimeondolewa katika ligi hiyo kutokana na kukosa kuheshimu ratiba ya ligi hiyo. Kulingana na sheria za fkf ukikosa kuhesimu ratiba mara tatu katika msimu moja kwa moja unashuka daraja.
Vilabu hivyo ni pamoja na Nameless FC, River Dale na Upcoming FC, zote kutoka Tana Delta. Timu hizi zimeondolewa katika ligi ya kaunti kwa kutohudhuria mechi tatu mfululizo huku nao Green stars wakiandika barua ya kujiondoa kwa ligi kutokana na mzozo wa ndani katika klabu.
Mechi zote zilizosalia na ambazo zinazohusisha klabu hizi sasa zimesimamishwa.
Aidha, kamati kuu ya usimamizi wa ligi hii inatarajiwa kutoa uamuzi wiki hii kuhusu mechi mbili kati ya Makere dhidi ya Eleven Stars na kisha mechi kati ya Intanna Giants na Matabule.

