Phil Foden, mchezaji wa klabu ya Manchester City aliachana na kambi yake ya timu ya taifa ya Uingereza huko Ujerumani ambako mashindano ya kombe la mataifa bara ulaya yanaendelea na kurejea nyumbani kwao Uingereza kwa ajili ya kuwa karibu na familia kipindi ambacho mke wake anajifungua.
Foden mwenye umri wa miaka 24 anatarajia kupata mtoto wake wa tatu hivyo aliomba ruhusa kutoka kwa uongozi wa The Three Lions kurejea nyumbani kwa ajili ya shuhuli hiyo.
Hayo yanajiri kipindi ambacho licha ya timu ya taifa ya Uingereza kukosa kuonyesha kiwango bora cha soka iilifuzu kutoka hatua ya makundi na sasa iko 16 bora na imepangwa kuvaana na Slovania, mechi ambayo imeratibiwa kuchezwa Jumapili.

