Timu ya taifa ya Kenya ya soka ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 Emerging Stars wanatarajiwa Kushuka dimbani jioni ya leo katika mechi yao ya kwanza ya mashindano ya COSAFA.
Mashindano hayo yanayoendelea Africa Kusini yalianza rasmi jana na yanaiweka Kenya katika chungu B kinachojumuisha Zambia, Comoros na Zimbabwe.
Emerging stars wanacheza mechi yao ya kwanza dhidi ya Zambia huku nyota kama vile Benson Omala akitarajiwa kushiriki sawa na makinda Adrine Kibet na Amos Wanjala ambao waliitwa kikosini baada ya kuonyesha soka zuri kwenye mashindano ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18.
Kulingana na viongozi wa soka nchini ni kuwa kikosi cha Emerging Stars kinalengwa kutumika kujenga timu ya taifa ya Harambe Stars itakayo shiriki kombe la Afcon mwaka 2027 ambapo Kenya watakuwa waandaaji pamoja na Tanzania na Uganda.

