Ujio wa udhamini wa ligi ya FKF kaunti ya kwale unazidi kuleta matumaini kwa vilabu vitakavyoshiriki ligi hiyo msimu ujao. Halmashauri ya Bandari KPA wiki hii ilitangaza udhamini wa shilingi milioni 18 kwa ligi ya kaunti hiyo kuelekea msimu ujao.
Kulingana na mwenyekiti wa FKF tawi la kaunti ya Kwale Hamisi Mwakoja ni kuwa udhamini huo sasa unalenga kusababisha msingi kujishindia takriban laki nne kwani shirikihso la soka linalenga kutenga zaidi ya milioni kutuza vilabu na wachezaji binafsi.
”Kutokana na udhamini huu tumetenga milioni nzima na zaidi kutuza wachezaji na timu, huenda bingwa wa ligi akajishindia laki nne” Alisema mwakoja.
Mwakoja amedokeza kuwa shirikihso la Kwale kwa kuhamia mfumo wa kidijitali kwenye kuendesha ratiba za ligi na masuala mbalimbali yalosababisha msimu kuenda bila lalama zozote kumesababisha kujishindia udhamini huo. Sasa ligi ya kaunti ya kwale msimu ujao itajulikana kama KPA Kwale County League.

