Rais wa shirikisho la soka la FKF nchini Nick Mwendwa amezidua rasmi kampeni ya kuleta wachezaji wa kike Viwanjani kama njia moja ya kuhamasisha taifa kuhusu umuhimu wa kufanya kinadada hapa nchini kujihusisha zaidi kwenye soka.
Kampeni hiyo ambayo ni ya kimataifa kwa ushirikiano na shirikisho la Fifa ilianza jana hapa nchini kwa kuandaliwa kwa Mashindano ya siku mbili katika uwanja wa Kasarani.
Nick Mwendwa ambaye ni Rais wa shirikisho anasema kwamba anaimani kubwa kuwa mradi huo utasaidia sana mwanadada hapa nchini katika makuzi ya talanta ambazo zinaweza kushamiri kimataifa.

