Lejendari wa timu ya taifa ya raga hapa nchini Collins Injera amesema kwamba Kenya ina safari ndefu katika kurekebisha uozo ulioko kwenye mchezo wa raga uliosababisha Kenya Shujaa kushuka daraja.
Amesema kuna mabao mengi ya kuzingatiwa ikiwemo masomo thabiti na kulea vipaji vya raga kutoka umri mchana tofauti na hali iliyoko kwa sasa ambapo hata hakuna hamasa ya kutosha kuhusu mchezo huo hapa nchini.
Amesema ukosefu wa vifaa vya michezo pamoja na makocha wa kutosha unachangia baadhi ya wachezaji kuanza kucheza mchezo huo wakiwa tayari ni wakubwa.
Mbali na hayo, amesema matatizo mengine kama malipo kuchelewa, miundo msingi mibovu pamoja na siasa nyingi na ufisadi vikiondolewa raga ya taifa hili inaweza kurejea kama ilivyokuwa miaka kadhaa ilopita.

