Timu ya taifa ya soka ya Kenya ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23, Emerging Stars wamerejea rasmi nchini baada ya kubanduliwa katika mashindano ya COSAFA yanayoendelea katika taifa la Afrika Kusini.
Kenya ilimaliza katika nafasi ya pili katika Kundi B ikiwa na alama sita, sawa na vinara Comoros waliokuwa na rekodi bora dhidi yao , na walikuwa wakiomba Namibia na Angola watoke sare au kupoteza mechi zao za mwisho za Kundi C ndiyo wao watinge nusu fainali.
Hata hivyo, Namibia iliizaba Ushelisheli 3-1 na kumaliza kileleni mwa kundi ikiwa na pointi saba, sawa na Angola ambao waliwatoa Lesotho kwa ushindi sawa na hio hapo jana.
Angola ilifuzu kwa nusu-fainali itakayo andaliwa Ijumaa, kama washindi wa pili bora.

