Winga wa timu taifa ya Senegal ambao pia ni mabingwa watetezi Krepin Diatta huenda akachukuliwa hatua za kinidhamu baada ya kulishutumu Shirikisho la Soka Afrika kwa kuwa fisadi kufuatia mabingwa hao watetezi kuondolewa kwenye kinyanganyiro cha AFCON kupitia mikwaju ya penalti dhidi ya wenyeji Ivory Coast wiki hii.
Diatta ambaye ni mshambuliaji wa timu ya Monaco huko Ufaransa alikasirishwa kwamba Senegal haikupewa penalti mapema katika kipindi cha pili, wakati Ismaila Sarr alipoangushwa kwenye eneo la hatari la Ivory Coast na beki Odilon Kossounou.
Simba wa teranga walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 wakati huo baada ya bao la mapema la Habib Diallo, lakini mwamuzi wa Gabon Pierre Ghislain hakupeana penalty hiyo wala kujaribu kwenda pembezoni mwa uwnaja kutumia VAR kupata maamuzi ya uhakika.
Sasa timu ya taifa ya Ivory Coast ambao ni waandaaji wa mashindano haya watacheza robo fainali Jumamosi dhidi ya Mali.

